Colgate Kuondoa Chunusi – Elewa Zaidi
Kwa miaka mingi watu wanaamini kuwa dawa ya meno ya colgate ina ufanisi mkubwa katika kuondoa chunusi usoni, shingoni, na hata mgongoni.
Na ingawa kwa kweli baadhi ya vitu vinavyotengeneza colgate vina nguvu ya kukausha viuvimbe na vipele kwenye ngozi, watu wengi hawana uhakika na usalama wa njia hii.
Vilevile, kuna dawa zingine na tiba mbalimbali salama na hakika za kuondoa chunusi kwenye ngozi yako. Wacha tuangazie swala kuu la usalama wa matumizi ya colgate kuondoa chunusi.
Je Matumizi ya Colgate Kuondoa Chunusi ni Salama?
Ingawa chanzo cha matumizi ya colgate kuondoa chunusi hakieleweki vizuri, watu hukisia kuwa matumizi haya yalianza kwa sababu zifuatazo:
- Dawa nyingi za meno huwa na kemikali inayojulikana kama triklosani. Kemikali hii ina nguvu za kuua bakteria zinazosababisha vipele na viuvimbe.
- Dawa za meno pia huwa na viungo vingine kama soda ya kuoka (baking soda), pombe kali (alcohol), na kadhalika zinazosaidia kukausha viuvimbe na chunusi sugu.
- Kulingana na utafiti wa Daktari mmoja mkuu wa ngozi (Tsippora Shainhouse), dawa za meno huwa na mentho inayosaidia kupunguza uchungu na mwasho kwenye chunusi na pia kupunguza viuvimbe.
Kwa kuzingatia sababu tulizozitaja hapo juu, ni bayana kuwa colgate ina nguvu ya kutibu na kupunguza chunusi. Lakini, kwa upande mwingine, kuna sababu zingine nyingi zinazokuhimiza kutotumia dawa ya meno ya colgate kama sulushisho lako la kwanza la kutibu chunusi.
1. Hii Ni Taarifa Iliyopitwa na Wakati
Utafiti uliofanywa na Shirika la Kimarekani la Kutoa Chakula na Dawa ulidhihirisha kuwa ingawa kemikali ya triklosani ina manufaa mengi katika kuzuia magonjwa ya ufizi, kemikali hii inaweza kuathiri dundumio.
Kwa hivyo, kampuni nyingi zimeacha kuongeza triklosani kwenye dawa zao za meno. Na ingawa bado kuna dawa zingine zilizo na kemikali hii, madhara yanayohusishwa na dawa hii yanapita manufaa yake katika kuzuia chunusi.
2. Si Tiba ya Kutegemewa
Wakati mwingine, dawa ya meno ya colgate huwa na mafanikio ya kuondoa chunusi kwa mtu mmoja. Lakini wakati mwingine, kemikali hizi zinaweza zikafanya ngozi yako kukauka kupita kiasi na kuvifanya vipele na vitundu vile kudhoofika.
Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi zetu floor ya 8 jengo la tanzanite park.