Chunusi Kwenye Uume
Chunusi zinaweza kutokea katika sehemu yoyote ya mwili iliyo na vitundu vya kutolea jasho. Hii ina maana kuwa viuvimbe hivi vinaweza kutokea hata kwenye uume wako.
Na kwa sababu hii ni sehemu nyeti, ni muhimu sana uwe makini kutambua dalili sahihi kabla ununue dawa za kujitibu.
Waathiriwa wengi wa chunusi kwenye uume huona aibu wanapopata tatizo hili na hata kukosa kulizungumzia. Lakini unapaswa kujua kuwa hili ni tatizo la kawaida linaloathiri watu wengi sana.
Na kwa hakika, lina tiba. Katika blogu hii tutakueleza mambo yote unayopaswa kujua kuhusu chunusi kwenye uume, hii ni pamoja na visababishi vyake, tiba, na jinsi ya kuzuia vipele hivi.
Visababishi vya Chunusi Kwenye Uume
Chunusi hutokea wakati vitundu vya kutolea jasho kwenye ngozi ya uume vinapozibwa na mafuta, bakteria, au seli zilizokufa. Dalili za chunusi kwenye ngozi hulingana na kitu kilichoziba vitundu vile vya kutolea jasho.
Dalili hizi pia hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kuna watu wanaopata viuvimbe vyenye usaha ilhali wengine hupata vipele tu. Chunusi zingine zina mwasho ilhali zingine haziwashi. Na watu wengine hupata viuvimbe vinavyosikika vigumu ilhali kwa wengine viuvimbe hivi huwa vyororo.
Mbali na haya, kuna mambo mengine mengi yanayosababisha kuwepo kwa chunusi kwenye uume. Kwa mfano:
· Uchafu
Wanaume wengi huwa na mazoea ya kutooga mara kwa mara. Uchafu na jasho zinapokusanyika kwenye sehemu zako za uume huwa huziba vitundu vya kutolea jasho kwenye ngozi na kusababisha chunusi. Siri ya kuzuia hili ni kuhakikisha kuwa unaoga mara kwa mara, angalau mara moja kila siku.
· Unyevunyevu kwenye suruali
Wanaoathirika zaidi na shida hii ni watu wanaoishi katika sehemu zenye joto jingi. Mwili wao hutoa jasho sana na jasho hili linapopita kiasi linaweza kusababisha unyevunyevu kwenye suruali.
Kwa vile bakteria huvutiwa sana na unyevunyevu, suruali inapokuwa majimaji huwa inachochea bakteria kujificha mle. Na kama tulivyotaja, bakteria ni mojawapo wa visababishi sugu vya chunusi.
Ili kuzuia unyevunyevu huu, chagua nguo za ndani za pamba. Hizi hukauka haraka na husaidia mwili wako kuwa kuna mzunguko wa hewa mzuri.
· Ngozi yenye mafuta mengi
Je wajua ngozi yako ni ya aina gani? Kuna aina tatu kuu za ngozi. Nazo ni: ngozi kavu, ngozi ya mafuta, na ngozi ambayo si kavu wala si ya mafuta. Ikiwa ngozi yako ni ya mafuta, ina maana kuwa tezi zako za kutoa mafuta ngozini hutoa mafuta mengi sana.
Mafuta haya yanapokuwa mengi kupita kiasi yanaweza kuziba vitundu vya kutolea jasho ngozini.
· Kuvaa suruali zinazobana
Siku hizi wanaume wengi, hasaa vijana, wanapendelea kuvaa suruali zinazobana sana. Ingawa zinapendeza, huenda zikakuletea maradhi ya chunusi. Hii ni kwa sababu, napovaa suruali zinazobana hewa huwa haipati kuzurura vizuri na hali hii hufanyiza ongezeko la bakteria kwenye ngozi.
Haimaaanishi kuwa usivae mavazi haya lakini hakikisha angalau unaporudi nyumbani unavaa mavazi yatakayoruhusu hewa kuzunguka vizuri, hasaa katika sehemu yako ya uume.
Pia ni muhimu kujua kuwa chunusi kwenye uume zinaweza kutokea hata kwa watu ambao hawashiriki tendo la ndoa.
Ila, ikiwa unashiriki ngono mara kwa mara, mbali na chunusi, upo katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa. Na kwa mara nyingi magonjwa haya huwa na dalili zinazosababisha viuvimbe kwenye uume sawa tu na chunusi.
Matibabu ya Chunusi Kwenye Uume
- Ikiwa umetambua kuwa una chunusi kwenye uume wako, usitie shaka. Mara nyingi chunusi hupona zenyewe na hautahitaji kutumia matibabu yoyote.
Njia bora zaidi ya kutibu chunusi kwenye uume wako ni kwa kutozisumbua. Usiziguseguse au hata kuzifinya kwani hili linaweza kufanya zikawa mbaya zaidi.
Unapozigusagusa na kuzivinya vipele hivi, kuna uwezekano mkubwa kuwa unazidisha nafasi za bakteria kuongezeka. Bakteria zitafanya viuvimbe vile kuongezeka tu. Badala yake, hakikisha sehemu ile ni safi na kavu kila wakati na baada ya siku kadhaa vipele vile vitapona vyenyewe.
- Pia kumbuka kuwa sehemu yako ya uume ni sehemu nyeti. Kwa hivyo, hauwezi ukatibu chunusi kwenye uume kwa kutumia dawa za kawaida za chunusi zinazouzwa madukani. Dawa zile huwa na nguvu nyingi na huenda zikasababisha mwasho zaidi au hata kuzidisha upele ule.
Ikiwa chunusi kwenye uume zitazidi kudhoofika hata baada ya kutozifinya au kuzisumbuasumbua na kuhakikisha kuwa uume wako ni safi na unabaki kuwa kavu kila wakati, unapaswa kupata ushauri wa mtaalamu wa magonjwa ya ngozi. Daktari huyu atakupa tembe za kumeza zinazokusudiwa kutibu chunusi sugu kwenye uume.
Visababishi Vingine Vya Uvimbe na Upele Kwenye Uume (Mbali na Chunusi)
Kama tulivyotaja hapo awali, si viuvimbe vyote kwenye sehemu yako ya siri ambazo ni chunusi. Wakati mwingine viuvimbe hivi huwa vinasababishwa na hali zingine. Hali hizi huenda zikwa na athari kubwa na ni muhimu upate matibabu upesi iwezekanavyo.
- Vipele na Viuvimbe Baada ya Kunyoa
Wakati mwingine mtu anaweza kupatwa na mwasho, wekundu, upele, au viuvimbe vidogovidogo punde tu baada ya kunyoa nywele kwenye uume. Viupele hivi hupona vyenyewe baada ya siku kadhaa.
Kwa hivyo, ikiwa huna mwasho wowote, ni bora uache sehemu ile ipone yenyewe. Lakini kama unawashwa sana, unaweza ukapaka losheni yenye unga wa shayiri.
Losheni hii itasaidia kumaliza mwasho huu upesi. Pia, ni vizuri kupaka losheni hii kila baada ya kunyoa ili kuzuia upele huu kutokea tena.
- Kaswede
Ugonjwa wa kaswede ni mojawapo wa magonjwa ya zinaa. Kaswede hutokea katika hatua nne tofauti. Katika hatua ya kwanza vipele vinaweza vikatokea kwenye uume wako na kuisha vyenyewe baada ya muda.
Ikiwa maradhi haya hayatagunduliwa na kutibiwa, ugonjwa huu huendelea kukua ndani ya mwili kwa muda mrefu, hata miaka, na vipele vingine kutokea tena kwenye uume wako. Tofauti na katika hatua ya kwanza, vipele hivi hutokea kwenye uume, mikono, miguu, nyayo, na hata kwenye viganja.
Ukipata kuwa una dalili hizi za ugonjwa wa kaswede, ni vizuri upate ushauri wa mtaalamu wa afya upesi iwezekanvyo. Ugonjwa wa kaswede ni hatari na athari zake zinaweza kufikia hata ubongo.
- Tezi za Tysoni
Tezi za tysoni ni tezi za kutengeneza mafuta ngozini zinazoonekana kwenye uume wako. Tezi hizi huonekana kama viuvimbe vidogo kwenye ngozi na kusababisha alama ndogo nyeupe au zenye rangi ya manjano.
Tulizotaja hapa juu ni baadhi tu ya visababishi vya viuvimbe unaofanana na chunusi. Kuna sababu nyingine nyingi. Kwa hivyo, ikiwahauna uhakika na dalili zako au hali inazidi kuwa mbaya, ni bora utembelee mtaalamu anayefaa.
Tembelea Mtaalamu wa Afya Upesi Ikiwa:
- Viuvimbe vinatoa usaha
- Upele umeenea sana
- Viuvimbe kwenye uume vinabadilika umbo na kipimo
Dalili hizi huenda zikawa za ugonjwa mwingine mwilini. Daktari wako atazichunguza na kuamua njia bora zaidi ya matibabu.
Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi zetu floor ya 8 jengo la tanzanite park.
You made some decent points there. I looked on the internet for the issue and located most individuals will go together with along with your website. Marcia Jerrie Prakash
my pleasure, thank you.
What a information of un-ambiguity and preserveness of valuable knowledge on the topic of unexpected emotions. Sibby Cooper Elfstan
thank you Torent.
Hi there, after reading this awesome article i am as well cheerful to share my familiarity here with friends. Sophronia Lazar Velda
you are welcome Bluray
Excellent Mark, I look forward to that and I share your admiration for Gregory Isaacs. Reba Gery Dorwin
thank you
Really informative blog article. Really thank you! Fantastic. Jana Georg Merrill
Your way of describing the whole thing in this piece of writing is actually fastidious, every one can without difficulty know it, Thanks a lot. Imogen Bret Gifford
Although sites we backlink to below are considerably not connected to ours, we really feel they are actually really worth a go via, so have a look. Loreen Donn Hickie
I truly appreciate this article. Really thank you! Really Cool. Florri Ignazio McMillan