Jinsi ya kuondoa chunusi mgongoni

Jinsi za Kuondoa Chunusi Mgongoni

Je una vipele au viuvimbe vidogovidogo mgongoni? Ungependa kujua njia rahisi na upesi ya kuondoa chunusi na vipele hivi? Katika blogu hii tutakuonyesha njia za kweli na zenye ufanisi mkubwa za kuondoa chunusi mgongoni.

Je Chunusi Mgongoni ni Nini?

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha viuvimbe au vipele kutokea kwenye ngozi. Vipele hivi hutokea hasaa kwenye uso, mgongo, shingo, au kifuani. Ingawa kwa kawaida vipele hivi huwa havina maumivu yoyote, wakati mwingine chunusi husababisha maumivu makali katika sehemu zilizoathirika.

Ni Nani Wanaoathirika Zaidi na Chunusi Mgongoni?

Takwimu za kuaminika zinaonyesha kuwa chunusi za mgongoni ni mojawapo wa magonjwa ya ngozi yanayoathiri kiasi kikubwa zaidi cha watu duniani. Kwa mfano, chunusi huathiri takriban watu milioni 17 nchini Marekani pekee.

Na ingawa vipele hivi vinaweza kuathiri mtu yeyote katika umri wowote, wanaoathirika zaidi ni vijana walio kati ya umri wa kubalehe, (kutoka miaka 12 hadi 25).

Chanzo cha Chunusi Mgongoni

Ngozi ya binadamu huwa na vitundu vya kutolea mafuta, jesho na vitu vinginevyo kutoka miilini yetu. Lakini mwili unapozalisha mafuta mengi kwenye ngozi kupita kipimo, mafuta haya huziba vishimo hivi na kusababisha vipele.

Mbali na hayo, chunusi za mgongoni pia zinaweza kusababishwa na:

  • Wingi wa bakteria ngozini
  • Aina fulani za matibabu
  • Mabadiliko ya homoni
  • Vinasaba (genetics), ambapo watu wa familia fulani huonekana kuathirika na chunusi kwa kiasi kikubwa
  • Mawazo mengi (stress)

Njia Nzuri na Salama za Kuondoa Chunusi Mgongoni

Kuna njia nyingi bora za kupunguza chunusi mgongoni, usoni, shingoni, na kifuani. Njia hizi hutofautiana kulingana na ukubwa la tatizo lile.

1.    Dawa za Chunusi Mgongoni

Kuna aina mbalimbali za dawa za kuondoa chunusi zinazouzwa madukani ya dawa na kwenye hospitali. Dawa hizi husaidia kufungua vitundu vya kutoa mafuta ngozini. Na kuna aina zingine zinazokusudiwa kuzidisha kipimo cha seli zinazotengeneza ngozi mpya mwilini.

Kwa kawaida, dawa za chunusi mgongoni hupatikana kama jeli, losheni, au krimu. Unashauriwa kupaka dawa hii angalau mara mbili kila siku au kama utakavyoshauriwa na daktari. Inaweza kuchukua muda wa wiki kadhaa kabla ya matokeo ya dawa zile kuonekana.

2.    Usiminye au Kusugua Vipele Hivi

Mara nyingi tunapokuwa na vipele hivi, tunaweza kufikiri kuwa tukivisugua au kuviminya huenda tutaviondoa viuvimbe hivi. Kinyume na haya, kusugua chunusi huleta maumivu kwenye ngozi na kusababisha ngozi kupata alama nyeusi za kudumu.

Ni muhimu pia upunguze muda unaoutumia kwenye jua. Jua linaweza kufanya chunusi zile kugeuka kuwa mbaya zaidi.

3.    Usitumie Vipodozi vinavyoziba vishimo vya ngozi vya kutolea jasho na mafuta

Ikiwa umeathirika na chunusi mgongoni, unashauriwa kupunguza matumizi ya mafuta ya mgando na hasaa ikiwa kuna joto jingi.

4.    Dumisha Usafi na Lishe Bora

Ukigundua kuwa una tatizo la chunusi mgongoni au kwenye sehemu yoyote ya mwili wako, unashauriwa kupunguza matumizi ya vyakula vinavyotengenezewa viwandani, vyakula vya maziwa, sukari, vyakula vilivyo na iodini nyingi hasaa chumvi, na upunguze matumizi ya pombe na tumbaku.

Hakikisha kuwa mlo wako unajumuisha matunda, vitamin B, mbogamboga za majani, nyuzinyuzi, na madini ya zinki na ukunywe maji ya kutosha kila siku. Kila mlo uwe kamili na upunguze kiasi cha mafuta unachotumia kupikia.

Na kwa sababu chunusi husababishwa na kuziba kwa vitundu ngozini, ni muhimu waathiriwa wadumishe usafi wakati wote. Hakikisha unaosha mwili na hasaa mgongo angalau mara mbili kila siku. Lakini uwe makini usitumie nguvu nyingi kuvisugua vipele hivi ili kuzuia maumivu zaidi.

5.    Tiba za Kiasili

Kuna njia salama na nafuu za kutibu chunusi mgongoni ukiwa kwenye starehe za nyumba yako. Na ingawa nyingi za njia hizi za asili hazijathibitiwa kisayansi, watu wengi wamezitumia na wamepata mafanikio makubwa.  Njia za kiasili ni salama na hazina athari zozote mbaya katika mwili wako.

  • Mchanganyiko wa asali na mdalasini uliosiagwa

Asali na mdalasini zina uwezo wa kuzuia na kuua bakteria. Na kama tulivyotaja hapo awali, mojawapo wa vitu vinavyosababisha chunusi ni bakteria. Paka mchanganyiko huu kwenye maeneo ya mgongo yaliyo na chunusi angalau mara moja kila siku.

Kutengeneza mchanganyiko huu:

  • Unahitaji mdalasini, asali, na mkebe wa kuchanganishia
  • Anza kwa kupima asali vijiko vitatu vya chai na kuiweka kwenye mkebe
  • Ongeza asali kijiko nusu cha chai
  • Changanya vizuri
  • Paka mchanganyiko huu kwenye sehemu za mgongo zilizo na chunusi. Subiri kwa muda wa dakika 10 hadi 30 na kisha uoshe sehemu zile kwa majimaji safi vuguvugu
  • Asali

Kwa miaka mingi asali imetumiwa kuua aina nyingi za bakteria. Vilevile, asali huua bakteria zozote zilizo kwenye ngozi. Pia itaboresha afya ya ngozi yako na kuifanya iwe nyororo na ya kupendeza.

Paka kiasi kidogo cha asali katika sehemu ya mgongo iliyoathirika. Na kwa sababu asali haina athari zozote mbaya za kiafya, unaweza kupaka asali mwilini mzima, kama jinsintu unavyopaka mafuta, ili kupata manufaa mwili mzima.

Iache asali itulie katika sehemu iliyo na chunusi kwa takriban dakika 30 au zaidi. Kisha oga kwa maji yenye joto la kadiri.

  • Matango

Matango yana manufaa mengi sana katika mwili wetu. Mbali na kuongeza maji yanayohitajika mwilini, pia yanapunguza uchovu, yanasaidia kuondoa msongo wa mawazo n.k.

Uchunguzi unaonyesha kuwa matango pia yanasaidia kuondoa chunusi mgongoni, usoni, na hata kifuani. Na hata watu wasio na chunusi wanaweza kutumia tango kuzipa ngozi zao afya.

Matumizi yake ni rahisi na matokeo yake ni hakika. Menya tango na ulikate katika viduara vidogo vidogo. Lala kitumbo na upake matango yale kwenye sehemu zilizoathirika na vipele hivi. Subiri takriban dakika 15 hadi 20 kisha usuuze kwa maji baridi.

Kwa matokeo ya upesi, paka tango mgongoni mara tatu kile siku.

  • Papai

Anza kwa kupondaponda papai lako ndogo. Kisha ulipake mgongoni sehemu zilizo na chunusi. Ili kupata manufaa zaidi, liache papai likae pahala pale kwa muda mrefu iwezekanavyo.  Kisha safisha mgongo  kwa kutumia maji yenye joto la kawaida. Paka mara tatu au nne kila siku,

Hatimaye

Kama utafuata ushauri tuliokupa hapa, kwa hakika, chunusi mgongoni zitaondoka kabisa. Lakini ni muhimu ujue kuwa chunusi zile zinaweza kuchukua muda kupona. Katika wakati ule, jambo la muhimu zaidi ni kupunguza mawazo.

Huenda chunusi zitapona lakini inaweza kuchukua wiki kadhaa kabla ya alama nyeusi zitakazobaki kuisha. Kumbuka kujiepusha na kemikali kali, dumisha usafi, kula mlo kamili, na punguza mawazo.

Na ingawa njia za kiasili huenda zisilete mafanikio kwa watu wote, dawa za chunusi kama vile sabuni, krimu, jeli, tembe za kumeza, na losheni zimeonekana kuleta mafanikio  makubwa. Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi zetu floor ya 8 jengo la tanzanite park.

Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi zetu floor ya 8 jengo la tanzanite park.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *