Njia Mbadala za Kuondoa Chunusi
Badala ya kubahatisha kuondoa chunusi kwa kutumia colgate, ni muhimu uzingatie njia zingine salama na hakika za kuondoa vipele hivi.
1. Dawa ya Meno ya Colgate Huenda Ikasababisha Mwasho Kwenye Ngozi Yako
Kumbuka kuwa colgate imetengenezwa kutunza meno ila si ya kutumia kwenye ngozi yako. Kwa hivyo, baadhi ya kemikali zilizotumiwa kutengeneza colgate ni kali sana na zinaweza kusababisha mwasho kwenye ngozi.
Kwa kawaida colgate ina kiasi kikubwa cha soda ya kuoka (baking soda). Kemikali hii inapopakwa kwenye ngozi huenda ikasababisha vipele na mwasho. Lakini athari za kemikali hizi pia hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Mtu mmoja anaweza kupatwa na mwasho mkali ilhali kwa mwingine, colgate yaweza ikawa yenye ufanisi.
· Dawa za Kutibu Chunusi
Kuna aina nyingi sana za dawa za kutibu ugonjwa wa ngozi wa chunusi zinazouzwa kwenye maduka ya dawa. Dawa hizi zinapatikana kama sabuni, mafuta, losheni, jeli, na kadhalika.
· Tiba za Kiasili za Chunusi
Pia kuna njia zingine nyingi na rahisi za asili za kutibu chunusi. Njia hizi ni nafuu na unaweza kujitengenezea dawa hizi ukiwa tu kwenye starehe za nyumba yako. Mifano mizuri ni:
I. Barafu
Mojawapo ya njia sala ya asili ya kupunguza chunusi ni kwa kutumia barafu. Barafu itasaidia kupunguza vipele na viuvimbe vya chunusi.
Utahitaji tu kuchukua kipande kidogo cha barafu yako na kukipitisha juu ya sehemu za uso au shingo zilizoathiriwa na chunusi. Fanya hivi mara kadhaa kwa mwendo wa wastani kwa muda wa takriban dakika nne au tano.
Fanya utaratibu huu kwa muda wa juma moja na utazame matokeo. Lakini ni muhimu ukumbuke kuosha sehemu ile kabla ya kupitishia barafu ili kupata matokeo bora.
II. Limau
Manufaa ya ndimu kwenye miili yetu ni mengi mno. Ndimu pia ina uwezo mkubwa wa kuondoa chunusi usoni, mgongoni, au kwenye sehemu nyingine ya ngozi yetu.
Limau huwa na kiwango kikubwa cha Vitamini C. Na kwa kawaida Vitamini C hutumika kama antibaiotiki inayouua na kuzuia bakteria wanaosababisha ugonjwa wa ngozi wa chunusi.
Ili kutumia limau kutibu chunusi utahitajika kulikata na nusu na kupaka maji ya limau lile kwenye sehemu zilizoathiriwa na chunusi. Lakini, kwa sababu limau lina ukali mwingi, unapaswa ulitumie kwenye ngozi yako mara moja au mbili tu kila wiki.
Ukilitumia kila siku, limau linaweza kudhuru ngozi yako na kufanya hali ya chunusi kuwa mbaya zaidi.
III. Kitunguu Saumu
Kitunguu saumu ni mojawapo ya dawa za asili zinazotibu maradhi mengi zaidi kwenye miili yetu. Na utafiti unadhihirisha kuwa kiungo hiki pia kina uwezo wa kutiba chunusi sugu kwenye uso, mgongo, shingo, na hata kwenye kifua.
Kisababishi kimoja cha chunusi kwenye ngozi ni mkusanyiko wa bakteria unaoziba vitundu vya kutolea jasho na mafuta ngozini. Kitunguu saumu nacho kina nguvu ya kipekee ya kuua bakteria hizi.
Kuna namna mbili za kutumia kitunguu saumu. Ya kwanza ni kutumia kutunguu hiki katika mapishi yako ya kawaida. Njia ya pili ni kukitwanga kitunguu kile na kukipaka kwenye sehemu zilizoathirka na chunusi.
Na ingawa kitunguu saumu kina manufaa makubwa katika kuondoa chunusi, unapaswa kukitumia kwa umakini sana. Unapokipaka moja kwa moja kwenye ngozi, kitunguu hiki huwa na nguvu sana. Nguvu hizi kali zinaweza zikaunguza ngozi yako na kufanya chunusi zile kuwa mbaya zaidi.
Njia bora ya kupunguza ukali huu ni kwa kuhakikisha kuwa unachanganya kitunguu saumu chako na maji kiasi kabla ya kukipaka kwenye ngozi yako.
IV. Tango
Tango ni tunda lililo na vitamini na potasiamu nyingi sana zilizo na manufaa mengi katika ngozi zetu. Watu wengi hutumia tunda hili kulainisha ngozi na kuifanya kupendeza zaidi.
Mbali na kufanya ngozi kuwa laini na yenye kupendeza, tango husaidia kuondoa vipele na chunusi kwenye ngozi. Matumizi yake ni rahisi sana. Utahitaji tu kuikata tango yako katika viduara vidogovidogo, kisha uviwekelee juu ya maeneo yaliyoathirika na chunusi.
Njia ya pili ambayo unaweza ukatumia tango kuondoa chunusi ni kwa kuisaga na kuchanganya majimaji yale na sukari kiasi. Kisha, tumia mchanganyiko ule kusugua sehemu zilizoathirika na chunusi kwa dakika mbili au tatu na umalizie kwa kusafisha sehemu ile kwa kutumia maji ya vuguvugu.
V. Tiba Zingine Salama za Asili
Tiba zingine ambazo unaweza kutumia kuondoa chunusi ngozini mwako ni kama asali, soda ya kuoka (baking soda), mvuke, papai, yai, mafuta ya zeituni, madalasini, uwatu (fenugreek), maganda ya ndizi, n.k.
Kumbuka
Ingawa ni kweli kuwa colgate ina nguvu za kuondoa chunusi, madhara yanayoweza kutokea huenda yakapita manufaa yale.
Pia, dawa ya meno huwa haileti mafanikio kwa watumiaji wote. Kwa hivyo usiitegemee dawa ya meno kama suluhisho lako la kwanza la kutibu chunusi. Kuna dawa za hakika na njia nyingine nyingi za asili zisizo na madhara yoyote.
Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi zetu floor ya 8 jengo la tanzanite park.